Job description
Msimamizi wa Mradi atawajibika kupanga, kuratibu, kusimamia na kufuatilia miradi ya ujenzi, ukarabati, majengo na maendeleo ya mali kutoka mwanzo hadi kukamilika, ikiwemo kusoma na kuandaa michoro ya usanifu na mipango ya ujenzi, kusimamia wakandarasi, wahandisi, wasanifu majengo, washauri na wasambazaji, kuandaa ratiba, bajeti, makadirio ya gharama na technical specifications, kufuatilia maendeleo ya miradi, gharama, muda na ubora wa kazi, kufanya ziara za maeneo ya ujenzi, kufuatilia masuala ya ardhi, upimaji, title deeds, valuation na nyaraka za mali, kushughulikia vibali na approvals za ujenzi kutoka mamlaka husika, kutunza kumbukumbu za miradi, kuandaa ripoti za maendeleo, kutambua changamoto na hatari za miradi pamoja na kupendekeza suluhisho ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati, ndani ya bajeti na kwa viwango vinavyohitajika.
Requirements & qualifications
Kusimamia na kuratibu miradi ya ujenzi, ukarabati, majengo na maendeleo ya mali kutoka mwanzo hadi kukamilika. Kusoma, kuandaa na kutafsiri michoro ya usanifu na mipango ya ujenzi. Kusimamia wakandarasi, mafundi, wahandisi, wasanifu majengo na washauri. Kuandaa ratiba za miradi, bajeti, makadirio ya gharama na specifications. Kufuatilia maendeleo ya mradi, gharama, muda na utendaji wa wakandarasi. Kufanya ziara za mara kwa mara kwenye maeneo ya ujenzi. Kufuatilia masuala ya ardhi, upimaji, mipaka, valuation, title deeds na nyaraka za mali. Kushughulikia vibali vya ujenzi na approvals kutoka mamlaka husika za Serikali. Kufuatilia matumizi ya fedha na kuhakikisha miradi inabaki ndani ya bajeti. Kutunza kumbukumbu za michoro, mikataba, vibali, ripoti na nyaraka za miradi. Kuandaa ripoti za maendeleo ya miradi. Kutambua hatari za miradi na kupendekeza suluhisho.
Benefits
Ajira ya muda wote (Full-time). Kazi inahusisha office-based na field-based responsibilities. Fursa ya kufanya kazi katika miradi ya ujenzi, property na development. Nafasi ya kushirikiana na architects, engineers, contractors, consultants na mamlaka za Serikali. Uzoefu wa kusimamia miradi na mali katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Salary & compensation
Contact information
About chuosmart
Tanzania\'s first platform to combine online education and digital commerce into a single, impactful ecosystem.